
Bintiye Obama afanya kazi mgahawani
Sasha Obama, 15, akifanya kazi
Sasha Obama, bintiye Rais wa Marekani Barack Obama,
ameamua kuacha 'starehe' za ikulu ya White House na kuanza kufanya kazi
katika mgahawa mmoja, vyombo vya habari nchini Marekani vinaripoti.Binti huyo wa umri wa miaka 15 ameanza kufanya kazi ya kuwahudumia wateja katika mgahawa mmoja ulioko Martha's Vineyard, Massachusetts.
Sasha, ambaye anatumia jina lake kamili, Natasha, aliandamana na maafisa sita wa ulinzi wa secret service siku yake ya kwanza kazini, gazeti la Boston Herald linaripoti.
Familia ya Obama hutembelea eneo hilo sana wakati wa likizo.
Picha zinazosambazwa zinamuonesha bintiye huyo mdogo wa Obama akiwa amevalia sare ya hoteli akifanya kazi.
Mfanyakazi mmoja katika mgahawa huo aliambia gazeti hilo la Herald: "Tulikuwa tunashangaa ni kwa nini kulikuwa na watu sita walikuwa wanamsaidia msichana huyu, lakini baadaye tukagundua alikuwa nani."
chanzo:bbcswahil

VIDEO: Mali za Freeman Mbowe zilivyotolewa nje ya jengo kisa deni la Bilioni
Kampuni ya udalali ikishirikiana na NHC ilitoa vifaa hivyo nje huku Wafanyakazi wa ofisi hiyo wakiwa kwenye hali ya kushangazwa ambapo meneja wa kitengo cha kukusanya madeni NHC alisema taratibu zote zilifatwa na Mbowe Hotels walishapewa notice sababu Mbowe anadaiwa BILIONI 1.72
Kampuni ya udalali iliyosimamia hilo zoezi imesema baada ya kuvitoa vifaa hivyo nje vikishachukuliwa kwa maelekezo ya NHC baada ya wiki mbili mmiliki asipolipa deni vitauzwa.
Ilisemekana Mbowe Hotels anao umiliki wa asilimia 75 ya jengo hilo lakini shirika la nyumba la taifa (NHC) limesema umiliki huo ulishafutwa, unaweza kutazama hii video hapa chini kutazama ilivyokua\
Subscribe to:
Posts (Atom)








